MRADI WA TESP KUWEKA MAZINGIRA MAZURI KATIKA UTOAJI WA ELIMU YA UALIMU VYUONI
Mratibu wa Mradi wa Kuendeleza Elimu ya Ualimu (TESP), Mwl. Cosmas Mahenge, ameelezea mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia mradi huo, ikiwemo ongezeko la vitabu na vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwa wakufunzi na wanafunzi.
Aidha, ameeleza kuwa Mradi huo umewezesha ujenzi na ukarabati wa miundombinu kama vile Maktaba, Maabara, na Madarasa, hatua inayoboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
Aidha, Mwl. Mahenge alibainisha kuwa Mradi huo umesisitiza Usawa wa ijinsia katika elimu ya ualimu na matumizi sahihi ya nishati safi ya kupikia, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuimarisha maendeleo endelevu.