Wakati ni huu tunaendelea kupokea Miswada kwa ajili ya Tuzo ya Mwalimu ya Uandishi Bunifu mpaka kufikia tarehe 31 Desemba 2024.
Tunaendelea kuwafikia wadau mbalimbali wa Sanaa na leo 10 Desemba 2024 Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu, Prof. Penina Mlama, amekutana na waandishi bunifu wa tamthiliya nchini kupitia Bodi ya Filamu ili kutoa elimu juu ya Tuzo hiyo.
kikao hicho kimehusisha viongozi wa Bodi ya Filamu, na waandishi wa tamthiliya.
Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo Prof. Mlama amesema tuzo hizo zinatoa nafasi ya kukuza lugha ya Kiswahili, utamaduni na maadili ya Kitanzania kupitia uandishi bunifu.
Tuzo ya 2024/25 inahusisha uandishi Bunifu katika Hadithi za Watoto, Ushairi, Riwaya, na Tamthiliya.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu, Dkt. Gervas Kasiga, aliongeza kuwa ushirikiano huu ni muhimu katika kukuza maandiko bora yatakayochangia maendeleo ya lugha na sanaa nchini.
Waandishi, hii ni fursa yetu kukuza lugha na utamaduni wetu..kwa maelezo zaidi tuandikie tuzonyerere@tie.go.tz