Imewasilishwa kwa DR. MAGRETH MATONYA- MKURUGENZI WA ELIMU MAALUM NA JUMUISHI - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Kwa Kujitolea Kwake kutaka kuhakikisha kuwa hakuna Mwanafunzi mwenye Mahitaji Maalum anayeachwa nyuma katika Kupata Elimu. Tuzo hii inasherehekea mchango wake mkubwa katika kusaidia Kuunda Mazingira Sahihi ya Elimu jumuishi nchini Tanzania.
Tuzo hii ilitolewa Siku ya Jumamosi, Tarehe 07, Mwezi wa 12, Mwaka 2024 @daressalaamserena katika Harambee ya Chakula cha Usiku ya Kuchangisha fedha kwa ajili ya Mradi wa USTAWI KWA KILA MTOTO- VIASHIRIA VYA USONJI uliozinduliwa siku hii na kiasi cha Shs 81,600,000 kilichangwa