Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi ina mchango mkubwa katika kuwezesha wananchi kupata maarifa, ujuzi na mielekeo stahiki kwa maendeleo endelevu.
Prof. Nombo ametoa kauli hiyo Oktoba 10, 2024 Mkoani Tabora akifungua Kongamano la Wadau wa elimu ambapo amesema Serikali inatambua kinadharia na vitendo umuhimu wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi.
"Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 Toleo la 2023 inasisitiza uyumbufu wa elimu na elimu bila ukomo ambayo inazingatia matumizi ya Sayansi na teknolojia kuhamasisha maendeleo binafsi" Alisema Prof. Nombo.
Aidha Nombo amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri Nchini kusimamia kikamilifu na kuweka msukumo wa program za Elimu ya Watu Wazima zinazotekelezwa katika maeneo yao.
"Tunahitaji kuweke mifumo madhubuti ya uendeshaji na usimamizi wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi" Alibainisha Prof. Nombo.