Kamati ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDC) leo Oktoba 18, 2024 imekutana Jijini Dodoma kupokea, Kujadili na kupitisha miongozo mbalimbali ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Kikao hicho kimeongozwa na Naibu Katibu Mkuu anaeshughulikia Sayansi Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Daniel Mushi akiwa na Wenyeviti wenza Naibu Katibu Mkuu Elimu Ofisi ya Rais- Tamisemi Atupele Mwambene, Mwakilishi wa UNICEF Simone Vis na Mwenyekiti wa TENMET Faraja Nyalandu.
Kamati hiyo ya Kisekta inahusisha wadau mbalimbali ikiwemo Wizara ya Elimu, OR -Tamisemi, Wizara ya Fedha , Wizara ya Mipango, Wadau wa Maendeleo, Sekta Binafsi, Asasi za kiraia na za Kidini.