Benki ya Dunia yapongeza kwa jitihada

Serikali imesema imeridhika na utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya kiuchumi (HEET) unaotekelezwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia katika Taasisi za Elimu ya Juu nchini kuputia ufadhili wa Benki ya Dunia ambao umefikia asilimia 55 katika kipindi cha Miaka Miwili na Nusu ya utekekezaji.



Akizungumza Oktoba 20, 2024 Jijini Dar es Salaam baada ya kikao na Wajumbe kutoka Benki ya Dunia, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Carolyne Nombo amesema kuwa Serikali imejidhatiti kuhakikisha Mradi huo unakamilika Kwa asilimia 100 kabla ya muda wa utekelezaji kuisha.



Mradi wa HEET unalenga kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia pamoja na kuweka miundombinu bora katika Vyuo inayoendana mazingira ya sasa na inakayowezesha kuongeza fursa na kutoa mafunzo yanaendana na Mageuzi ya elimu na kuchagiza maendeleo ya kiuchumi nchini.



"Tupo katika hatua nzuri na karibu kila eneo la mradi limeguswa katika kipindi hiki cha Miaka miwili na nusu ya utekelezaji mradi, na tunaelekea kukutana na wadau wote kufanya tathimini ya maeneo ambayo bado yanahitaji uangalizi wa haraka ili kufikia malengo kama ilivyokusudiwa" amesema Prof. Nombo.



Naye Kiongozi wa Ujumbe wa Benki ya Dunia Prof. Roberta Basset Malee amepongeza Serikali hasa katika usimamizi wa Mradi huo na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano ili kuhakikisha unakamilika kama ulivyopangwa.



Moja ya eneo kubwa la utekekezaji mradi huu ni ujenzi wa Kampasi 16 za Vyuo vikuu katoka mikoa mbalimbali nchini ikiwemo kikoa ya Kigoma, Mtwara, Njombe, Tanga na Mara