Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni, na Michezo imeendelea na vikao kupokea taarifa mbalimbali.



Leo Oktoba 17, 2024 jijini Dodoma Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewasilisha taarifa ya Utendaji Kazi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) na Taarifa ya maendeleo ya Ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi na Chuo cha VETA Mkoa wa Songwe.



Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Husna Sekiboko na Menejimenti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikiongozwa na Mhe. Prof. Adolf Mkenda Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.