Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Caroylne Nombo amesema kuwa Wanafunzi wanaosoma Mkondo wa Amali watalazimika kusoma masoma matano ya lazima pamoja na moja la fani.



Akizungumza Septemba 26, 2024 Mkoani Ruvuma wakati wa uwasilishaji wa mada ya Mageuzi katika Sekta ya elimu kwa wajumbe wa Mafunzo ya Matumizi ya Matokeo ya Sensa kwa Viongozi wa Kisiasa Wanawake Tanzania, amesema kuwa fani kuu katika mkondo huo ni 15.



Prof. Nombo ameyataja masomo hayo ya lazima kuwa ni Hesabu, Kiingereza, Elimu ya Biashara, Lugha ya Mawasiliano, Hisitoria ya Tanzania na Maadili ambalo litafundishwa kwa kiswahili

2