Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali inaendelea kupanua Mfuko wa Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ili kuwezesha watoto wakitanzania kusoma bila wasiwasi wowote.



Akizungumza Mkoani Ruvuma Sept 27, 2024 mara baada kuzindua shule ya Sekondari ya wasichana Samia Suluhu Hassan iliyopo Namtumbo Ruvuma, amesema kuwa Serikali itaendeleea kuwekeza katika sekta ya elimu na kuwataka wanafunzi kuhakikisha wanasoma kwa bidii masomo ya Sayansi na kutumia vizuri mifumo ya kitehama.



Shule hii ni moja kati ya Shule 26 za Wasichana za Mchepuo wa Sayansi zinazojengwa nchi nzima kupitia Mradi wa SEQUIP unatekekezwa na Wizara ya Elimu na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.