Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo ikiongozwa na mwenyekiti wake Mh. Husna Juma Sekiboko imeendelea na ukaguzi wa miradi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inayotekelezwa nchini ambapo imeshuhudia ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Shimbo Mkuza ambayo imejengwa kupitia mradi wa SEQUIP.



Katika mwaka wa fedha 2022/23 Halmashauri ya Mji Kibaha kupitia shule ya Sekondari Nyumbu ilipokea kiasi cha sh. 528,998,425 kwaajili ya Ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Shimbo Mkuza iliyopo kata ya Mkuza Halmashauri ya Mji Kibaha Mkoa wa Pwani na mradi huu ulianza rasmi tarehe 05 Agosti 2023 na kukamilika tarehe 30 Oktoba 2023 na hadi kufikia sasa jumla ya majengo 25 yamekamilika na yanatumika.



Ni wanafunzi 281 wanasoma katika shule, wavulana ni 149 na wasicharia ni 132 na shule hii imeweza kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule mama ya Sekondari Nyumbu na shule za Jirani za Msangani government na shule ya Sekondari Simbani.