Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema ni muhimu kuwekeza katika elimu na kuongeza ujuzi wa wafanyakazi ili kuinua kiwango cha rasilimali watu katika kuchochea maendeleo kiuchumi.
Waziri Mkenda amesema hayo Agosti 29, 2024 Jijini Dar es Salaam akimwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Phillip Mpango katika Mahafali ya nne ya Wahitimu wa Program ya Mafunzo kwa Wakuu wa Taasisi na Mashirika, ambapo amesema program hiyo ina manufaa chanya katika kuongeza tija ya utendaji, nani kwa kuzingatia hilo ndio sasa Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatekeleza mageuzi makubwa ya Elimu kuhakikisha ina ijenga umahiri na ujuzi kwa Wahitimu.
"Viongozi mahiri katika sekta za Umma na Binafsi wanayo nafasi kubwa ya kuboresha utendaji na maisha ya watu ambao ni nguzo katika kuchagiza maendeleo, hivyo Serikali itaendelea kufanya kazi kwa karibu na Taasisi ya Cohort ili kufikia malengo yanayokusudiwa kujenga rasimali watu bora kama mtaji katika maendeleo" Alisema Waziri Mkenda.