Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekutana na wadau ili kupokea maoni ya Rasimu ya Mpango wa Maendeleo wa Sekta ya Elimu 2021/22 - 2025/26 yatakayowezesha kufikia malengo, shabaha na kutekeleza mikakati ya kuendeleza Sekta ya Elimu nchini.



Akizungumza Agosti 19, 2024 Jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa mkutano wa wadau hao, Dkt. Wilson Charles Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia amesema kuwa rasimu ya mpango huo imeandaliwa na kikosi kazi maalum, hivyo mkutano huo unalenga kupata maoni kutoka kwa wadau ili kuiboresha rasimu hiyo na iweze kutekelezwa kwa ufanisi.



Dkt. Charles amesema kuwa ni muhimu kwa wadau hao kutoa maoni kwa kuzingatia mabadiliko katika sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya Sera ya Elimu na Mafunzo, Mitalaa na pia kuzingatia taarifa ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.