Taasisi zimehimizwa kujipanga ili kutoa huduma bora kwa wananchi na hatimaye kuongeza mchango wa sayansi, teknolojia na ubunfu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Hayo yamesemwa hii leo tarehe 17 Julai 2024 na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojaia Prof. Carolyne Nombo akiwa nchini Afrika Kusini ambapo amepata nafasi ya kutembelea taasisi ya utafiti wa viwanda ya Afrika Kusini.
Aidha, Katika ziara hiyo Katibu Mkuu alipata nafasi ya kueleza mafanikio ya ushrikiano kati ya nchi hizi mbili katika utafiti hususani kupitia uanzishwaji wa vigoda vya utafiti vya eOR-TAMBO.
Aidha, Katibu Mkuu alipata nafasi ya kutembelea maabara za kisasa katika taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na maabara za kuendeleza teknolojia na bidhaa za wabunifu pamoja na wajasiliamali wakiwemo waliopo katika mfumo usio rasmi