Serikali imesema makubaliano ya ushirikiano kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Idara ya Sayansi na Ubunifu ya Afrika Kusini imewezesha kutekelezwa kwa miradi ya pamoja ya kitafiti katika vyuo vikuu na kuendeshwa kwa makongamano ya pamoja ya kujengeana uwezo na mifumo ya udhibiti, kuanzishwa kwa vituo vya teknolojia na uanzishwaji wa vigoda vya OR-TAMBO.



Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo wakati akizungumza na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara Sayansi na Ubunifu ya Afrika Kusini Bw. Daan du Toit ambapo amesema kuwa ni muhimu kwa pande zote kusimamia na kutekeleza makubaliano hayo na ameombakuwa na mashirikiano zaidi katika Elimu ya Juu, na Masuala ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (TVET).



Kwa upande wake Bw. Daan du Toit, ameipongeza Tanzania kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kutekeleza makubaliano ya ushirikiano na kuahidi kuendeleza mashirikiano hayo