Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema mageuzi ya uchumi yanahitaji kuwekeza katika nguvu kazi ya Taifa hasa kundi la Vijana linalotegemewa kushiriki katika sekta mbalimbali za uzalishaji.



Mkenda ameeleza hayo Julai 12, 2024 Jijini Dar Salaam wakati akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Phillip Mpango kufungua Kongamano la Pili la Mwaka la Uchumi (EST) la Jumuiya ya Wachumi Tanzania 2024, ambapo amesema maudhui ya Kongamano hilo yana uhusiano mkubwa na mageuzi ya Elimu nchini.



Aidha amesema Serikali inatekeleza juhudi mbalimbali katika kusaidia maendeleo nchini pamoja na kufanya mageuzi makubwa ya elimu na uboreshaji wa miundombinu ili kuwezesha utolewaji wa elimu bora kwa Watanzania.