Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Juni 25, 2024 ameshiriki Mkutano ulioandaliwa na Benki ya Dunia na kushirikisha wadau wote wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu nchini (Development Partners in Education) Jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho kilichohudhuriwa pia na Katibu Mkuu Profesa Carolyne Nombo, Naibu Katibu Mkuu Profesa James Mdoe, wakurugenzi wengine wa Wizara na Ofisi ya Rais Tamisemi kilijadili mwelekeo wa uwekezaji katika miradi ya Elimu nchini.
Akizungumza katika kikao hicho Prof. Mkenda amewashukuru wadau wa maendeleo kwa kufadhili miradi mbalimbali na kuelezea umuhimu wa kuendelea kushirikiana ili kuwezesha utekelezaji wa mageuzi ya Elimu hususani kuimarisha mafunzo ya mkondo wa Amali kwa kuwekeza katika rasimali hitajika ikiwemo walimu.
Kwa upande wake Nathan Belete, Mkurugenzi Mkazi (country director) wa Benki ya Dunia amesema wataendelea kushirikiana na Serikali nia ni kuona matokeo chanya ya ujifunzaji katika shule na Vyuo pamoja kuongeza fursa za mafunzo katika ngazi mbalimbali za elimu ikiwemo kuimarisha mafunzo kwa walimu