Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ally Abdulgulam Hussein leo Juni 21, 2024 wametekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ya kutaka Wizara hizo zikutane kujadili namna mbalimbali za kuboresha Elimu Nchini.



Katika kikao hicho Waziri Mkenda amesema katika mpango wa Ujenzi wa Shule mia moja za Amali,shule moja itajengwa Zanzibar, Pemba jimbo la Mkojani, huku akieleza kuwa mpaka kufikia January 2025 Shule ishirini na sita zitakuwa zimekamilika.



Kwa upande wake Naibu Waziri Ally Abdulgulam ameshukuru kwa idadi kubwa ya wanafunzi wa elimu ya juu wanaonufaika na mkopo ambapo idadi hiyo imekuwa ikiongezeka kufikia wanafunzi 800 mwaka wa fedha 2023/24.



Vile vile wamejadiliana namna ya kuendeleza Chuo cha Kimataifa cha India Institute of Technology (IITMZ) na kukitangaza ili kifahamike na kupata wanafunzi wengi zaidi.