Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda, amewasili katika viwanja vya Shule ya Sekondari Tabora Wavulana, kwa ajili ya kufunga mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania UMITASHUMTA.



Mashindano hayo yaliyoanza Juni 05,2014 yanahitimishwa rasmi leo Tarehe 15, 2024 ikiwa ni takriban siku 10 zilizoshuhudia michezo mbalimbali ya wanafunzi wa shule na msingi ikichezwa katika viwanja mbalimbali shule za Sekondari Tabora wasichana na wavulana, lamoja na Chuo cha Uhazili Tabora.



Michezo iliyohusika katika mashindano hayo ni pamoja na soka wavulana na wasichana, soka maalum, mpira wa kikapu,wavu, Netiboli, Mikono, Sanaa za Michezo, Riadha, na Goalball ambao ni mchezo maalum kwa wenye uoni hafifu.



Kuhitimishwa kwa michezo ya UMITASHUMTA 2024 ni mwanzo wa kuanza kwa mashindano ya UMISSETA 2024 yatakayohusisha shule za Sekondari kutoka mikoa yote ya Tanzania ambayo yanatarajiwa kuanza Mkoani Tabora June 17,2024.



Mashindano ya UMITASHUMTA & UMISSETA 2024, yanaandaliwa na kuratibiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo.