Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo yupo katika Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga katika ziara Chuo cha Ualimu Korogwe na Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe.
Akizungumza na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Michael Kipaya Prof. Nombo amemueleza kuwa baada ya kuanza utekelezaji wa Mitaala iliyoboreshwa ni muhimu sana kuwaelimisha Wazazi na Walezi juu ya mabadiliko ya elimu na hivyo amewataka kushiriki katika kutoa elimu na uhamasishaji kuanzia ngazi za Halmashauri na Wilaya ili jamii iweze kufahamu umuhimu wa mabadiliko hayo kwa manufaa ya jamii na Taifa.
Aidha Prof. Nombo amewakaribisha Wakazi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kushiriki Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yaliyoanza Mei 25 hadi 2025.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Bw. Michael Kipaya ameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kusimamia sekta hiyo pamoja na kufuatilia utekelezaji wa Mitaala mipya ya Elimu