Na
WyEST
Nairobi , Kenya
Aprili, 2024
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia Mhe Qs Omar Juma Kipanga akifuatilia ufunguzi wa Kongamano la sita la Partneship for Skills in Apllied Sciences and Engineering Technology (PASET) na (RSIF) Regional Scholarship and Innovation Fund linalofanyika Nairobi Kenya.
PASET ni ushirika unaofadhiliwa na Benki ya Dunia ukiwa na wanachama 25 kutoka nchi za Afrika ikiwemo Tanzania.
Kongamano la sita linalenga kubadilishana uzoefu na kuzihamasisha nchi wanachama kuchangia katika kutatua changamoto ya upungufu wa ujuzi na maarifa katika nyanja za sayansi tumizi, uhandisi na teknolojia.
Tanzania imekua ikinufaika na PASET kupitia scholashipu na miradi ya utafiti katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Taasisi ya Afrika ya sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela ( NM-AIST).