Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughukia Watoto (UNICEF) April 24, 2024 limekabidhi vifaa vya kielimu kwa ajili ya Wanafunzi na Walimu wa Shule zilizoathiriwa na mafuriko yanayotokana na mvua zinazoendelea katika Wilaya ya Kibiti na Rufiji Mkoani Pwani na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya Kibiti Kanali Joseph Kolombo.



Utekelezaji wa ahadi hiyo, umekuja siku chache baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda kueleza kuwa Wadau mbalimbali watashirikiana na Serikali kuchangia vifaa mbalimbali na huduma kuwezesha wanafunzi walioathiriwa na mafuriko hayo kuendelea na masomo katika shule wanazopangiwa.
Hatua hii ni utekelezaji wa Mkakati wa Kukabiliana na Majanga katika sekta ya Elimu.



Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na mahema yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 120 kila moja yatakayofungwa katika makambi, seti za vifaa vya sayansi zitakazo nufaisha Wanafunzi 360, vifaa vya kufundishia kwa ajili ya walimu 400, seti za vifaa vya kufundishia madarasa ya Awali pamoja na vifaa vya michezo vitakavyo nufaisha Wanafunzi 360