Katika kuendelea kuwajengea uwezo watekelezaji mbalimbali wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023, Wizara inaendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo Wathibiti Ubora wa Shule.



Mafunzo hayo yaliyoanza Aprili 15, 2024 katika Chuo cha Ualimu Morogoro yana lengo la kuwawezesha wathibiti hao kufahamu juu ya mwongozo wa upimaji shirikishi wa matokeo ya ujifunzaji kulingana na kitita cha ubora wa ufundishaji wa elimu ya awali.



Mafunzo haya yatawajengea uwezo katika kutekeleza kwa ufanisi jukumu la usimamizi, ufatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa sera