Serikali imeanza ujenzi wa vyuo vya Ufundi na Ufundi Stadi (VETA) katika Wilaya 64 ambazo hazikuwa na vyuo hivyo pamoja na Chuo cha Mkoa wa Songwe.
Haya yameelezwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga Machi 16, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Chuo cha ufundi na Ufundi Stadi cha wilaya ya Kinondoni kinachojengwa Mabwepande.
Naibu Wazori ameielezea Kamati hiyo kuwa katika awamu ya kwanza ya ujenzi wa vyuo hivyo vya wilayi Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 100 kwa ajili ga ujenzi wa majengo tisa katika vyuo vyote vya wilaya pamoja na kujenga majengo yote ya Chuo cha Mkoa wa Songwe.
Akizungumza Ujenzi wa Chuo cha Ufundi cha Wilaya Kinondoni amesema kimetengewa zaidi ya shilingi bilioni 1.4 na kwamba mpaka sasa kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 300 zimetolewa na majengo yote tisa yamejenhwa na yapo hatua ya msimgi
Naye Mthibiti Ubora wa Shule wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni ambaye ndiye msimamiizi wa ujenzi wa chuo hicho Naitwa Mghumba amesema kiwa ujenzi katika eneo la mradi inakabiana na changamoto ya maji na kuletea kuongezeka kwa gharama za ujenzi kwa kuwa wanapaswa kununua maji.
Mwenyikiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamadyna Michezo Mhe. Husna Sekiboko ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolonia kuipatia kamati hiyo taarifa kamili ya ujenzi wa vyuo hivyo ili ione namna ya kusaidia kutafuta suluhu ya changamoto zinazojitokeza