Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Nyaraka za Usimamizi wa Maafa zitakuwa ni za kitaifa na hivyo taasisi na wizara mbalimbali na wadau waliopewa majukumu katika nyanja za biolojia, kemikali na nyuklia watazitumia kwa kuzingatia mahitaji ya Taasisi zao.



Prof. Mkenda amesema hayo Machi 14, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Nyaraka za Usimamizi wa Maafa na zoezi la utayari wa kukabiliana na dharura za Kemikali na Mionzi ambapo amesema kuwa lengo kuu ya mipango hiyo ni kuwa na mikakati ya pamoja kama taifa ya kukabiliana na majanga hayo



Akizungumza kuhusu mafunzo ya Utayari wa dharura za Kemikali na Mionzi amesema kuwa yalilenga kuwapa washiriki maarifa na ujuzi wa kukabiliana na vutisho kikemikali, kibailojia, kiradiojia na kinyuklia na kusaidia juhudi za kuzuia na kukabiliana na majanga hayo.