Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Program ya Kuboresha Kada ya Ualimu ni muhimu sana katika maendeleo ya Elimu ya Tanzania na kwamba inaenda sambamba na Sera ya Elimu ya 2014 Toleo la 2023 inayosisitiza uendelezaji wa Walimu.



Prof. Mkenda amesema hayo Machi 13, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa program hiyo, ambapo amesema Serikali itaendelea kuwajengea uwezo Walimu kwa kutoa elimu bila ukomo ili kuwaongezea ujuzu na mbinu za ufundishaji.



Amesema Serikali inatambua umuhimu wa Walimu hivyo inalenga kuhakikisha kada hii inakuwa bora zaidi na kuwapatia mazingira bora ya kufanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuwa na makazi.



"Mradi huu umekuja wakati muafaka ambapo tumeanza utekelezaji wa Sera Toleo la 2023 ambayo inahimiza kuwa na Walimu bora na mahiri. Walimu wanafanya kazi kubwa, tulinde heshima ya Ualimu ili elimu iendelee kuwa bora, " Mkenda