Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Elimu, Utamaduni na Michezo imeitaka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kujitangaza kuwezesha vijana kujinga ili kupata mafunzo mbalimbali yanayotolewa.
Akizungumza Januari 20,2024 wakati wa ziara ya Kamati hiyo katika Ofisi za Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam Kaimu Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Musa Siima amesema Taasisi ya Watu Wazima inafanya kazi nzuri ya kutoa elimu kwa njia mbadala kwa vijana walio nje ya mfumo rasmi ambayo inawasaidia vijana kutimiza ndoto zao za elimu.
Ameongeza kuwa Taasisi hiyo ambayo ina programu mbalimbali za kutoa mafunzo nje ya mfumo usio rasmi ina wajibu wa kuhakikisha vijana wote waliotoka kwenye mfumo rasmi wa elimu wanapatiwa elimu na mafunzo ya ujuzi ili kuwawezesha kuchangia katika maendeleo ya nchi.