Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameiambia Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Elimu, Utamaduni na Michezo kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha watoto wote waliotoka nje ya mfumo rasmi wa elimu kwa sababu zozote zile wanarudi shule ili kupata elimu na ujuzi na kutimiza ndoto zao za kuwaletea maendeleo binafsi na ya Taifa.



Prof. Mkenda ameongeza kuwa wizara kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) wanatarajia kufanya tathimini ya kwanza ya watoto waliokatisha masomo kwa sababu mbalimbali na kisha kurudi shuleni baada ya serikali kutoa waraka wa kuwarudisha ili kuona kama wana changamoto zozote na jinsi ya kuboresha mafunzo yao.



" Tumekubaliana na UNICEF tufanye programu ya kwanza kwa kushirikiana ya kutathimini wanafunzi waliorudi shuleni baada ya tangazi la serikali , tutakaa na kuongea nao kuangalia changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi" amesema Waziri huyo

Ameongeza kuwa kuna programu mbalimbali za mafunzo kwa watoto na vijana walikatika masomo kupitia FDC, Taasisi ya Elimu ya Watu wa zima na wengine wamerifi katika mfumo rasmi.