Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda leo Disemba 2023 jijini Dar es Salaam ameshiriki mazungumzo yaliyoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE) Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa GPE Laura Frigenti.
Kupitia mazungumzo Viongozi hao wameeleza dhamira ya Serikali ya Tanzania katika kutekeleza mageuzi ya elimu na kutambua mafanikio yaliyotokana na mchango wa Shirika hilo na kuangalia namna litakavyoweza kusaidia maeneo mengine, ikiwemo katika utekelezaji wa Sera ya elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 Toleo la 2023 na mabadiliko ya mitaala ya elimu.