Tunapiga vita na kulaani wizi wa Mitihani, naomba tushirikiane kwa pamoja kuhakikisha tunadumisha uadilifu, uaminifu kulijenga Taifa letu kwa kupata Wahitimu mahiri.

Ni kauli yake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza leo Novemba 30, 2023 jijini Dar es Salaam katika Ufunguzi wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).