Na WyEST
DSM
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Carolyne Nombo tarehe 27 Novemba, 2023 ameongoza Kikao kati ya Vyuo vikuu vya Ardhi, Dodoma, Mzumbe, Dar es Salaam, Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi (VETA), Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi na ujumbe kutoka Chuo cha Jiingxi cha taaluma za kigeni nchini China.
Kikao hicho kilichofanyika Jijini Dar eS salaam kimelenga kujenga ushirikiano baina ya pande hizo mbili katika kukuza na kuendeleza taaluma za uhandisi, maendeleo ya ujuzi, teknolojia na ubunifu katika tasnia ya ufundi.
Vyuo vya elimu ya ufundi nchini China vimepiga hatua katika ukuzaji na uendelezaji ujuzi kwa vitendo, kujenga stadi za kazi, utendaji viwandani na bunifu za kiteknolojia hivyo kupitia makubaliano yatakayoingiwa Vyuo hapa nchini vitapata uzoefu na hivyo kuandaa wahitimu wenye stadi na mahiri zinazoendana na soko la ajira kitaifa na kimataifa.