Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga amewataka wasimamizi wa Ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Same kuongeza umakini na kasi ya ujenzi ili mradi huo ukamilike kwa wakati na kwa ubora.

Ameyasema hayo leo Novemba 16, 2023 alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi ikiwa pamoja na kutatua changamoto ambapo amesema lengo la kuhakikisha ifikapo mwezi wa 10 mwaka 2024 ujenzi uwe umekamilika.



Naibu Waziri huyo amezitaka kamati za ujenzi kuwa na utaratibu wa kuweka kumbukumbu zote za shughuli zinazoendelea kwenye mradi huo ikiwemo kumbukumbu za manunuzi ili kurahisisha ufuatiliaji na kutatua changamoto zinazojitokeza



Mhe. Kipanga pia amesisitiza wasimamizi wa mradi huo kuhakikisha mafundi wanafuata vipimo vilivyopo kwenye michoro ya ujenzi wa majengo hayo.

Serikali imetenga shilingi billioni 2.6 kujenga chuo hicho ikiwa ni moja ka ya Vyuo 64 vya VETA Wilaya vinavyojengwa nchini kote.