Mwenyekiti wa Baraza la Usimamizi wa Taasisi ya Elimu Watu Wazima (TEWW) Dkt. Naomi Katunzi ameishukuru serikali kupitia Wizara ya Elimu chini ya Mradi WA SEQUIP, kwa kuipatia taasisi hivyo jumla ya fedha TZS. Bilioni 5.7 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa na vituo vya Elimu.
Dkt. Katunzi ametoa pongezi hizo Oktoba 12, 2023 wakati akizungumza kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Juma la Elimu ya Watu wazima Viwanja vya Maili Moja Wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani.
"Hii imewezesha kuwapa fursa mabinti waliopata ujauzito kurejea Shule na katika mazingira bora zaidi ya kujifunza, ni imani yangu kuwa tutaweza kutimiza ndoto zao" Alisema Daktari. Katunzi.
Pia amewashukuru wadau wa maendeleo UNICEF, UNESCO na Shirika la Kimataifa DVV kushiriki kikamilifu kufanikisha Maadhimisho hayo.
"Kwa muda huu UNICEF, kupitia Mradi wa Elimisha Mtoto wanafadhili utekelezaji wa MEMKWA kwenye mikoa ya Tabora, Kigoma na Songwe.