Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula amewata Viongozi na wakufunzi katika Chuo cha Ualimu Katoke kuwa wabunifu katika ufundishaji ili kuzalisha walimu mahiri.

Ameyasema hayo Septemba 11,2023 alipotembelea Chuo hicho kukagua Miundombinu mbalimbali ya Chuo iliyojengwa na kufanyiwa ukarabati.



Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Mwl. Michael Ntwale ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwekeza katika Elimu ya Ualimu hususani katika Chuo cha Ualimu Katoke.

Chuo hicho kimeweza kuongeza udahili hadi kufikia wanachuo 438 baada ya Uboreshaji na kwamba kimejikita katika kutoa mafunzo ya ualimu wa awali na Msingi