Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda tarehe 07.09.2023 wamekutana na kujadili namna ya kuongeza idadi na ubora wa wahadhiri katika Taasisi za Elimu ya Juu za Umma.
Kikao hicho kimefanyika Jijini Dodoma na kimehudhuriwa na katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof .Carolyne Nombo na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Xavier Daudi na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara hizo.
Pamoja na jitihada nyingine zinazofanywa na Serikali kuhakikisha utoshelevu na ubora wa Wahadhiri katika Taasisi za Elimu ya Juu, viongozi hao wamejadili na kukubaliana kuunda kikosi kazi shirikishi kitakacho jumuisha wadau mbalimbali husika na Taasisi za Elimu ya Juu ili kufanya uchambuzi wa kina na kutoa mapendekezo