Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefanya kikao cha pamoja na Tume ya Mipango kujadili mwelekeo wa Sekta ya Elimu kulingana na Rasimu ya Sera ya Elimu na Mafunzo 2014 Toleo 2023 na Mabadiliko ya Mitaala kwa kuzingatia Mipango mbalimbali ya Kitaifa na maelekezo wa Nchi.
Kikao hicho kimefanyika jijini Dar es Salaam Septemba 6, 2023 kwa lengo la kuhakikisha mpango na mkakati wa utekelezaji wa Sera hiyo inazingatia mipango ya serikali ili kuwezesha utekelezaji wake pindi Sera itakapopitishwa.
Kwa upande wa Wizara ujumbe uliongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo, na kwa upande wa Tume ya Mipango Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Ndg. Lawrence Mafuru.
Wajumbe wengine waliohudhuria ni Mwenyekiti wa Kamati ya mapitio ya Sera Prof. Joseph Semboja na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabadiliko na uandaaji Mitaala Prof. Makenya Maboko, na baadhi ya wajumbe wa Kamati hizo.