Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Mradi wa Kuboresha Vyuo vya Ualimu (TESP) imefanya maboresho makubwa ya miundombinu ya Chuo cha Ualimu Mpwapwa ambayo yameongeza kwa kiwango kikubwa udahili na ufaulu wa Walimu Tarajali.
Maboresho hayo yamehusisha ujenzi wa Maktaba kubwa yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 100 kwa wakati mmoja, ujenzi wa maabara za sayansi za Fizikia, Kemia na Biolojia pamoja na ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia ikiwemo vya maabara na madawa.