Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo Leo Agosti 22, 2023 Jijini Dodoma, ameendelea na kukutana na Idara mbalimbali za Wizara ambapo amekutana na watumishi wa Idara ya Uthibiti Ubora wa Shule ili kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha kasi ya kuhudumia wadau.
Prof. Nombo ameitaka Idara hiyo kuandika maandiko ya Miradi ambayo itawezesha Idara kutatua changamoto za rasilimali fedha na kuacha kutegemea fedha kutoka Miradi mingine.
Aidha Katibu Mkuu huyo amesema Idara hiyo ina muundo mzuri ya uendeshaji shughuli zake nakuwataka kuimarisha mahusiano ya kiutendaji kazi Kati yake na Ofisi ya Raisi TAMISEMI hasa katika ngazi ya Wilaya ambapo Ofisi za wathibiti Ubora zipo ili kuwezesha kufanya Kazi kwa Ufanisi.
Naye Naibu katibu Mkuu Elimu Dkt. Franklin Rwezimula ameitaka Idara hiyo kujikita zaidi katika kuongeza uwezo wa matumizi ya TEHAMA katika utendaji wa Kazi zao.