Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula amehimiza matumizi ya TEHAMA kwenye mafunzo ya Llfundi Standi ili kuendana na kasi ya ukuaji wa Teknolojia na mahitaji ya soko kwa wahitimu wa mafunzo hayo.

Ametoa rai hiyo wakati wa Ziara yake mkoani Kilimanjaro alipotembelea Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA Moshi na kujionea wanafunzi Wakiendelea na mafunzo kwa vitendo.

Pia Dkt. Rwezimula amewaasa wanafunzi wa kike kupenda Fani za Ufundi na kusema zinajenga ujuzi moja kwa moja. Pia amewaasa wanafunzi wa chuo hicho kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza malengo waliojiwekea na kuongeza rasilimali watu yenye ujuzi na utaalamu wa amali nchini