1. UTANGULIZI
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anatangaza nafasi za mafunzo ya Ualimu kwa ngazi ya Stashahada ya Ualimu wa Sekondari. Waombaji wa mafunzo haya ni wahitimu wa Kidato cha SITA wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (I-III). Wizara inakaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali na visivyo vya Serikali kwa kuzingatia sifa zilizobainishwa katika tangazo hili.
2. SIFA ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU
Sifa za jumla za kujiunga na Mafunzo ya Ualimu Tarajali ngazi ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Sekondari ni wahitimu wa Kidato cha Sita wenye ufaulu wa Daraja la I-III kwa kiwango cha “Principal Pass” mbili (02) za masomo yanayofundishwa katika shule za sekondari Kidato cha I-IV. Aidha, kwa waombaji ambao moja ya “Principal Pass”mbili ni somo la Uchumi “Economics”, wanaweza kuomba kozi za fani ambazo ni Michezo (Physical Education and sports), Muziki, Sanaa za Ufundi (Fine Arts), na Sanaa za Maonesho (Theatre and Performing Arts).
3. AINA ZA MAFUNZO
Jedwali lifuatalo linaonesha aina ya mafunzo ya Ualimu, sifa za kujiunga, vyuo vinavyotoa mafunzo hayo na muda wa mafunzo