Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, inawaalika watanzania wenye ubunifu, ugunduzi na maarifa asilia kushiriki katika Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) kwa mwaka 2022.
Usajili umeanza tarehe 27 Disemba, 2021 na utakamilika tarehe 10 Februari, 2022. Mashindano hayo yatahusisha makundi saba ya wabunifu ambayo usajili wake unaratibiwa na kusimamiwa na taasisi mbalimbali.
Usajili wa kundi la KWANZA na la PILI, linalohusisha Vyuo Vikuu na Taasisi za Utafiti na Maendeleo utafanywa na COSTECH;
Usajili wa kundi la TATU na la NNE, linalohusisha Vyuo vya Ufundi Stadi na Mfumo usio Rasmi utafanywa na VETA na Ofisi za Halmashauri nchini;
Usajili wa kundi la TANO, linalohusisha Vyuo vya Kati utafanywa na NACTE & DIT; na Usajili wa kundi la SITA na la SABA, linalohusisha shule za Msingi na Sekondari utafanywa na Ofisi za Maafisa Elimu wa Mikoa husika. Mwongozo na Fomu zinatolewa kupitia wasimamizi walioainishwa au wavuti ya https://makisatu.costech.or.tz
Tathmini ya ubunifu uliowasilishwa itafanyika ili kupata washindi watakaoshiriki katika Wiki ya Kitaifa ya Ubunifu Tanzania kwa mwaka 2022.
Kwa maelezo zaidi wasiliana kwa simu namba 0754-520176 au 0784-865994 au tuma baruapepe kwenda makisatu@moe.go.tz.