NGAZI YA ASTASHAHADA YA UALIMU ELIMU YA AWALI, MSINGI NA STASHAHADA YA UALIMU ELIMU YA SEKONDARI 

KATIKA MASOMO YA SAYANSI, BIASHARA NA HISABATI KWA MWAKA WA MASOMO 2023/2024

 

  1. UTANGULIZI

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia anatangaza nafasi za mafunzo ya Ualimu kwa ngazi ya Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali, Msingi na Stashahada ya Ualimu Elimu ya Sekondari katika masomo ya Sayansi, Biashara na Hisabati (miaka 03). Waombaji wa mafunzo haya ni wahitimu wa Kidato cha Nne wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (I-III). Wizara inakaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali na visivyo vya Serikali kwa kuzingatia sifa zilizobainishwa katika tangazo hili.

  1. SIFA ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU

Sifa za jumla za kujiunga na Mafunzo ya Ualimu Tarajali ngazi ya Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi ni wahitimu wa Kidato cha Nne wenye ufaulu wa Daraja la I-III. Aidha, sifa za kujiunga na Mafunzo ya Ualimu Tarajali ngazi ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Sekondari katika masomo ya Sayansi, Biashara na Hisabati (miaka 03) ni wahitimu wa Kidato cha Nne wenye ufaulu wa Daraja la I-III kwa kiwango cha  ufaulu wa kiwango cha  “C” katika masomo matatu katika hayo, mawili yawe ni ya tahasusi  za masomo ambayo mwombaji anaomba kusomea.

  1. AINA YA MAFUNZO NA SIFA

Jedwali lifuatalo linaonesha aina ya mafunzo ya Ualimu, sifa za kujiunga, vyuo vinavyotoa na muda wa mafunzo.

  1. MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA ASTASHAHADA YA ELIMU YA AWALI NA MSINGI

Na.

AINA YA MAFUNZO

SIFA ZA KUJIUNGA

VYUO

MUDA WA MAFUNZO

1

 

 

 

 

Astashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi

  1. Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha daraja la I-III. Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya Hisabati,English na Sayansi.

 

  1. Aliyehitimu Kidato cha VI ni sifa ya nyongeza.

 

 

Bustani TC, Ilonga TC, Kabanga TC, Katoke TC

Kitangali TC, Kinampanda TC, Mandaka TC

Mtwara (U) TC, Mhonda TC, Murutunguru TC

Mpuguso TC, Singachini TC,

Tandala TC, Tarime TC Vikindu TC, Nachingwea TC, Ndala TC, Mamire TC, Shinyanga TC, Marangu TC,Tabora TC, MonduliTC, Sumbawanga TC na Dakawa TC

 

 

 

 

Miaka 2

2

 

 

 

Astashahada  ya Ualimu Elimu Maalum

  1. Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha Daraja la I-III. Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya Hisabati na Sayansi

 

  1. Aliyehitimu Kidato cha VI ni sifa ya nyongeza.

 

Patandi TC,

Kabanga TC na Mpwapwa TC

 

 

 

 

Miaka 2

 

 

 

 

3

 

 

 

Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali

  1. Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha Daraja la I-III   Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya Sayansi, Hisabati na Englsh.

 

  1. Aliyehitimu Kidato cha VI ni sifa ya nyongeza.

Kinampanda TC, Nachingwea TC, Mhonda TC

Tarime TC, Vikindu TC, Mpuguso TC, Mandaka TC, Singachini TC

Murutunguru TC, Kabanga TC, Bustani TC

Ndala TC, Katoke TC, Bunda TC, Sumbawanga TC, Tabora TC

 

 

 

 

Miaka 2

 

 

 

 

4

 

 

 

Astashahada ya Ualimu Elimu kwa Michezo 

  1. Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha Daraja la I-III. Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu masomo ya sayansi na hisabati.

 

  1. Aliyehitimu Kidato cha VI au uzoefu katika michezo ni sifa ya nyongeza.                                

 

 

Tarime TC, Mtwara (K) TC, Ilonga TC, Tabora TC

 

 

 

 

Miaka 2

 

 

 

 

5

Astashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi (English Medium)

  1. Ufaulu wa Kidato cha IV kwa kiwango cha Daraja la I-III. Kipaumbele kitatolewa kwa waliofaulu somo la English

 

  1. Aliyehitimu Kidato cha VI ni sifa ya nyongeza.                               

 

Dakawa TC, Marangu TC, Tabora TC

 

 

 

 

 

 

Miaka 2

 

 

 
  1. MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA YA UALIMU ELIMU YA SEKONDARI MASOMO YA SAYANSI, BIASHARA NA HISABATI

 

1

 

Stashahada ya Ualimu Sayansi, Biashara na Hisabati

 

Ufaulu wa Kidato cha IV kwa Daraja la I-III kwa kiwango cha  ufaulu wa “C” katika masomo matatu  kati ya hayo mawili yawe ni ya tahasusi  za masomo ambayo mwombaji anaomba kusoma. Masomo hayo ni:  Basic Mathematics, Biology,Food &nutrition, Chemistry, Physics, Agriculture Science, Information and Computer Studies (ICS) na Computer Science, Commerce, Accountant.

 

Monduli TC, Butimba TC, Kleruu TC, Songea TC, Tukuyu TC, Kasulu TC, Mpwapwa TC, Morogoro TC, Korogwe TC, Tabora TC Mandaka TC (kwa masomo ya Sayansi na Hisabati)  na Sinyanga TC (kwa masomo ya Biashara)

 

 

 

 

 

Miaka 3

 

   

                 C.     MAFUNZO YA UALIMU KAZINI (ASTASHAHADA YA ELIMU MSINGI ELIMU MAALUMU)

 

 

Na.

AINA YA MAFUNZO

SIFA ZA KUJIUNGA

CHUO

MUDA WA MAFUNZO

 

 

1

Astashahada Elimu Maalum (Mafunzo kazini) Msingi

Mwalimu kazini (ambaye ameajiriwa katika shule za Serikali au shule za binafsi) aliyepitia mafunzo ya Ualimu Astashahada, Stashahada au Shahada kwa ufaulu wa angalau somo moja la Sayansi katika mtihani wa Kidato cha Nne na awe na uzoefu wa kazi ya Ualimu usiopungua miaka miwili (2)

Patandi TC

Miaka 2

         
 

UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI

  1. Wahitimu wa kidato cha nne wenye sifa zilizobaizinishwa kwenye tangazo hili  wanaruhusiwa kutuma maombi.
  2. Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Ualimu vya Serikali wanatakiwa kujisajili na kufanya maombi kielektroniki kupitia mfumo wa udahili wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia (tcm.moe.go.tz).
  3. Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu kwa vyuo visivyo vya Serikali watume maombi yao moja kwa moja katika vyuo wanavyotaka kusoma na vyuo husika viwasilishe sifa za waombaji Baraza la Mitihani Tanzania kwa uhakiki.
  4. Mwombaji  wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali atachagua tahasusi tatu (03) kwa kuanza na ile anayoipenda zaidi.
  5. Waombaji wa nafasi za mafunzo walio kazini wanapaswa kuwa wamehitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti, Stashahada au Shahada.
  6. Walimu Kazini watapaswa kuwasilisha barua ya ruhusa kutoka kwa waajiri wao mara baada ya kuripoti chuoni;
  7. Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu yatatolewa kupitia “account” aliyotumia mwombaji kuomba mafunzo ya Ualimu (kuanzia 05/07/2023) na katika Vyuo vya Ualimu walivyochaguliwa.  
  8. Barua na fomu  za kujiunga na Mafunzo zitatolewa kupitia tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (www.moe.go.tz) na Chuo atakachopangwa mwombaji kwa kutumia anuani yake. Waombaji wote wanashauriwa kuandika anuani kamili, barua pepe na namba ya simu inayopatikana kwa mawasiliano zaidi.
  9. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30/06/2023.   

Tanbihi: Masomo ya Dini hayatatumika kama kigezo cha sifa ya kujiunga na Mafunzo ya Ualimu.

 

                                                                                           

                                                                                            Prof. Calolyne I. Nombo

                                                                                                  KATIBU MKUU