Serikali, wadau na watalaam wa sekta ya elimu wamekutana Septemba 19,2024 jijini Dar es Salaam na kujadili vipaumbele katika kuboresha Sekta ya Elimu 

Kati ya aeneo yaliyotajwa kuwa ya kipaumbele katika mjadala huo ni uendelezaji wa taaluma ya ualimu na ajira, mazingira ya utoaji elimu na uwajibikaji.

Kwa upande wa Taaluma ya Ualimu imeelezwa kuwa Serikali imeanza utekekezaji wa Mradi wa  GPE (TSP) wenye thamani ya Dola 167 milioni (zaidi ya Sh454.04 bilioni), unafadhiliwa na Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE).

Hayo yameelezwa leo, Septemba 19, 2024 katika kikao cha wadau kilichohudhuriwa na  Naibu Katibu Mkuu (Elimu) na  Wizara  Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Atupele Mwambene katika kikao cha wadau juu ya mapitio ya tathmini ya vipaumbele vya nchi juu ya mradi huo.

Amesema tayari kuna kikosi kazi cha pamoja kilichofanya tathmini tangu mwaka 2022 na kuonyesha vipaumbele vya nchi katika sekta ya elimu.

Meneja Programu Mwandamizi wa GPE kutoka Ubalozi wa Sweden, Stella Mayenje amesema kupitia mradi huo Tanzania ilinufaika awali kwa kupata Dola 84 milioni (zaidi ya Sh228.3 bilioni).

Hatua ya Tanzania kupata kiasi hicho kidogo, amesema ilitokana na kutotimiza baadhi ya masharti na hivyo kinachofanyika sasa ni kuhakikisha inayatimiza.