Wizara kupitia Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) inatangaza ufadhili wa masomo ya fani za nyuklia kwa wanawake katika ngazi ya Umahiri kupitia Programu ya IAEA Marie Sklodowska Curie Fellowship (MSCFP) kwa mwaka wa masomo 2024/25 hadi 2025/2026.
Kwa mujibu wa tangazo kipindi cha maombi kwa mwaka 2024 kimefunguliwa kuanzia tarehe 12 Julai, 2024 na kitafungwa tarehe 30 Septemba 2024. Kwa taarifa zaidi kuhusiana na ufadhili huo fuatilia kupitia
https://www.iaea.org/services/key-programmes/iaea-marie-sklodowska-curie-fellowship-programme/information-for-applicants