1.0 UTANGULIZI
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inapenda kuujulisha umma wa Watanzania kuwa kiungo cha kuombea masomo nchini Algeria kwa mwaka 2025/2026 kwa Shahada ya Kwanza, Shahada ya Umahiri na Shahada ya Uzamivu kupitia mtandao umefunguliwa.
2.0 UTARATIBU WA KUOMBA NAFASI ZA MASOMO
Taarifa za Vyuo Vikuu mbalimbali nchini Algeria zinapatikana kupitia jukwaa la kidigitali la “Study in Algeria”.
Kwa waombaji wanaopenda kuomba fursa za masomo waombe kupitia kiunganishi kifuatacho: (https://studyinalgeria.dz). Maombi ya wasilishwe kabla au ifikapo tarehe 30 Juni 2026.
Imetolewa na:
Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Aprili 2026

