1. UTANGULIZI
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatangaza nafasi za mafunzo ya Ualimu ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali, Msingi na Elimu Maalumu. Mafunzo yatakayotolewa ni Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali, Msingi, Elimu Maalumu (Miaka 02) na Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) katika masomo ya sayansi, hisabati na TEHAMA. Waombaji wa mafunzo ya Ualimu ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali, Msingi na Elimu Maalumu (miaka 02) ni wahitimu wa Kidato cha sita wenye ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi la Tatu (I-III) na Walimu wahitimu wa Elimu ya Ualimu ngazi ya Astashahada.
Waombaji wa mafunzo ya Ualimu ya Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) katika masomo ya sayansi, hisabati na TEHAMA ni wahitimu wa kidato cha nne wenye ufaulu wa Daraja la kwanza hadi la tatu (I-III). Mafunzo haya yatatolewa katika vyuo vya Serikali na Vyuo visivyo vya Serikali. Vyuo vya ualimu visivyo vya Serikali vitatoa mafunzo haya baada ya kuwasilisha maombi na kupata kibali cha Kamishna wa Elimu. Wizara inakaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali na visivyo vya Serikali kwa kuzingatia sifa zilizobainishwa katika tangazo hili.
2. SIFA ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU
a) Sifa za kujiunga na Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali, Msingi na Elimu Maalumu (Miaka 02) ni:
- Wahitimu wa Kidato cha Sita wenye ufaulu wa Daraja la I-III kwa kiwango cha “Principal Pass” mbili (02). Aidha, kwa waombaji waliosomea masomo ya Economics, Commerce na Book Keeping waombe kozi ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Awali.
- Walimu waliohitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya Astashahada (Cheti) ya Ualimu Elimu ya Awali, Msingi au Elimu Maalumu. Aidha, waombaji wa mafunzo watakaochaguliwa kwa sifa hii watapangwa kwenye michepuo kulingana na ufaulu wao katika Mtihani wa Taifa wa Ualimu ngazi ya Astashahada.
b) Sifa za kujiunga na Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) katika masomo ya Sayansi, Hisabati na TEHAMA ni wahitimu wa Kidato cha nne wenye ufaulu wa Daraja la I-III kwa kiwango cha alama “C” au zaidi katika masomo matatu, mawili kati yake yakiwa ni: BasicMathematics, Biology, Chemistry, Physics, Information and Computer Studies au Computer Science.
- AINA YA MAFUNZO NA VYUO VINAVYOTOA MAFUNZO
Jedwali lifuatalo linaonesha aina ya mafunzo ya Ualimu (kozi) na vyuo vinavyotoa mafunzo husika.
- STASHAHADA YA UALIMU ELIMU YA AWALI, MSINGI NA ELIMU MAALUMU (MIAKA 02)
Na. | AINA YA MAFUNZO (KOZI) | VYUO VINAVYOTOA MAFUNZO |
1 | Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi mchepuo wa Sayansi ya Jamii (kwa kutumia lugha ya kiswahili) | Mhonda, Murutunguru, Vikindu na Bustani |
2 | Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi mchepuo wa Sayansi ya Jamii (kwa kutumia lugha ya kingereza) | Mpuguso na Shinyanga
|
3 | Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi mchepuo wa Sayansi ya jamii na lugha ya kiswahili (kwa kutumia lugha ya kiswahili).
| Bunda |
Stashahada ya Ualimu Elimu Maalumu ( kwa kutumia lugha ya kingereza) | Patandi na Mpwapwa
| |
5 | Stashahada ya Ualimu Elimu Maalumu ( kwa kutumia lugha ya kiswahili) | Kabanga, Patandi na Mpwapwa |
6 | Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi mchepuo wa Sayansi na Hisabati (kwa kutumia lugha ya kingereza) | Kasulu, Mandaka na Mamire |
7 | Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi mchepuo wa Sayansi na Hisabati (kwa kutumia lugha ya kiswahili) | Kitangali, Sumbawanga, Tandala |
| Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali (kwa kutumia lugha ya kingereza) |
Dakawa na Nachingwea |
10 | Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali (kwa kutumia lugha ya kiswahili)
| Kinampanda, Katoke na Singachini. |
11 | Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi mchepuo wa lugha (Kingereza, Kiswahili, Kifaransa na Kichina) | Marangu |
12 | Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi mchepuo wa Sanaa na Michezo (kwa kutumia lugha ya kingereza) | Butimba |
13 | Stashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi mchepuo wa Sanaa na Michezo (kwa kutumia lugha ya kiswahili)
| Ilonga na Tarime |
- STASHAHADA MAALUMU YA UALIMU ELIMU YA MSINGI KATIKA MASOMO YA SAYANSI, HISABATI NA TEHAMA (MIAKA 03)
Na | AINA YA MAFUNZO (KOZI) | VYUO VINAVYOTOA MAFUNZO |
1 | Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi katika masomo ya Sayansi, Hisabati na TEHAMA (Miaka 03) | Monduli, Butimba, Klerruu, Songea, Tukuyu, Kasulu, Mpwapwa, Morogoro, Korogwe naTabora. |
4. UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
(i) Wahitimu wa kidato cha nne, kidato cha sita na walimu waliohitimu Astashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi, wenye sifa zilizobainishwa katika Tangazo hili wanaruhusiwa kutuma maombi;
(ii) Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Ualimu vya Serikali wanatakiwa kujisajili na kutuma maombi kielektroniki kupitia mfumo wa udahili wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (https://tcm.moe.go.tz);
(iii) Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu kwa vyuo visivyo vya Serikali watume maombi yao moja kwa moja katika vyuo wanavyotaka kusoma na vyuo husika viwasilishe sifa za waombaji Baraza la Mitihani Tanzania kwa uhakiki;
(iv) Mwombaji wa mafunzo ya Ualimu ya Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi (Miaka 02) atachagua kozi tatu (03) kwa kuanza na ile anayoipenda zaidi;
(v) Mwombaji wa mafunzo ya Ualimu ya Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) atachagua tahasusi tatu (03) kwa kuanza na ile anayoipenda zaidi;
(vi) Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali yatatolewa kwenye mfumo kupitia “account” aliyotumia mwombaji kuomba mafunzo ya Ualimu (kuanzia tarehe 09/08/2024) na katika Vyuo vya Ualimu walivyochaguliwa;
(vii) Fomu za kujiunga na Mafunzo zitatolewa kupitia tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (www.moe.go.tz) na Chuo atakachopangwa mwombaji kwa kutumia anuani yake. Waombaji wote wanashauriwa kuandika anuani kamili, barua pepe na namba ya simu inayopatikana kwa mawasiliano zaidi; na
(viii) Majibu na fomu za kujiunga na Chuo kwa watakaochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu visivyo vya Serikali yatatolewa na vyuo husika.
(ix) Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 08/09/2024.