BOOST Primary Student Learning Program

Malengo ya Uanzishwaji wa Programu (MUP)

Malengo ya Programu ni kuboresha upatikanaji fursa sawa katika ujifunzaji bora wa Elimu ya Awali na Msingi Tanzania Bara. BOOST ni sehemu ya Mpango wa Lipa Kulingana na Matokeo katika Elimu awamu ya pili (EPforR II) na inachangia utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Sekta ya Elimu wa miaka mitano 2021/22 hadi 2025/26.

Matokeo Muhimu na Kuimarisha Mfumo:

Matokeo Muhimu

  • Vyumba vipya vya Madarasa 12,000 kujengwa na vifaa vya shule vinavyohusika katika maeneo yenye uhitaji zaidi
  • Vituo 800 katika shule za msingi/Vituo vya Walimu kuanzishwa na kuendelezwa kwa ajili ya utoaji wa mafunzo kwa njia ya TEHAMA kupitia maktaba mtandao/kielektroniki na Mfumo wa Usimamizi wa Ujifunzaji kimtandao
  • Shule za Msingi 6,000 kuwezeshwa kutekeleza Programu ya Shule ya Msingi Salama
  • Madarasa 12,000 ya Elimu ya Awali yaliyoboreshwa pamoja na njia bora za ufundishaji vikiwemo Vifaa vya ujifunzaji
  • Kuongezeka kwa uwiano wa uandikishaji wa wanafunzi wa Elimu ya Awali kutoka asilimia 76.9 hadi asilimia 85;
  • Kuongezeka kwa uwiano wa uandikishaji wa wanafunzi wa Elimu ya Awali kutoka asilimia 57.5 hadi asilimia 65.6 kwa Halmashauri zilizo katika kundi la robo ya chini;
  • Kuongezeka kwa kiwango cha wanafunzi kubaki shuleni katika Halmashauri zilizo katika kundi la robo ya chini kutoka asilimia 55.9 hadi asilimia 66.24;
  • Asilimia 50 ya wanafunzi wa Darasa la Pili kufikia kiwango cha chini cha kumudu stadi za Kusoma na Kuandika na asilimia 35 katika Kuhesabu.
  • Ushiriki wa walimu katika Mpango wa Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA) kufikia asilimia 50

Kuimarisha Mfumo Katika

  • Takwimu, mipango, ufuatiliaji na tathminiMaendeleo ya Sera yanayotokana na ushahidi
  • Maendeleo ya sera yanayotokana na uthibitisho
  • Ujenzi wa miundombinu kwa kushirikisha jamii
  • Uwezo wa kitaifa katika uandaaji wa mitaala na upimaji katika ujifunzaji
  • Umahiri wa matumizi ya TEHAMA kwa wanafunzi na walimu wa shule za msingi
  • Mfumo wa kitaifa wa Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA)
  • Kuimarisha Maktaba Mtandao na Mfumo wa Usimamizi katika Ujifunzaji
  • Halmashauri zinazozingatia utawala bora katika elimu
  • Usimamizi wa shule
  • Maendeleo ya elimu yanayozingatia mazingira na hali za kijamii

VIASHIRIA VYA MALIPO (DLIS)

Mradi wa BOOST unafuata utaratibu wa ufadhili unaozingatia Lipa kulingana na Matokeo; kwa hivyo utoaji wa fedha utategemea kufikiwa kwa matokeo yaliyokubaliwa kama yatakavyothibitishwa na Wakala Huru (IVA) aliyeajiriwa chini ya Mpango huu. Jumla ya viashiria (DLIs) nane na viwango vyake vya ufadhili vimebainishwa hapa chini

Eneo la Matokeo

DLI

 

IDA US$ millioni

Kuboresha mazingira ya Ujifunzaji na Ufundishaji

DLI-1

Utekelezaji wa Mpango wa Uendelezaji wa Miundombinu ya shule unaozingatia mahitaji

150

DLI-2

Utekelezaji wa Mpango wa Shule za Msingi salama

50

DLI-3

Kuongezeka kwa asilimia ya uwiano wa uandikishaji wa wanafunzi wa Elimu ya Awali

50

Kuboresha ujuzi wa walimu na ubora wa ufundishaji darasani

DLI-4

Utekelezaji wa njia bora na matumizi ya vifaa stahiki vya kufundishia na kujifunzia katika madarasa ya Elimu ya Awali

 

50

DLI-5

Halmashauri zinatekeleza Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA) katika ngazi za shule na kupitia Vituo vya Walimu

60

DLI-6

Idadi ya Shule za Msingi na Vituo vya Walimu (TRC) vinavyotekeleza mtaala wa TEHAMA katika kufundishia na kujifunzia vinavyowezeshwa kupitia mfumo wa usimamizi wa ujifunzaji.

50

Kuimarisha utoaji wa fedha na ugatuzi wa huduma

DLI-7

Utengaji wa bajeti kwa ajili ya Kuwezesha shughuli muhimu za Programu na kuhakikisha kuwa kiwango cha bajeti kinadumishwa au kuongezwa

20

DLI-8

Idadi ya Halmashauri zinazokidhi vigezo vya utawala bora katika elimu

50

Jumla

 

 

480

DLI 1: Utekelezaji wa Mpango wa Uendelezaji wa Miundombinu ya shule unaozingatia mahitaji

Mwaka 1: Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI zitaidhinisha Mpango wa Taifa wa Uendelezaji wa Miundombinu ya Shule za Msingi ambao utabainisha mahitaji na kuweka mpango wa ujenzi. Mpango huo utajumuisha ukarabati na upanuzi wa shule zilizopo pamoja na ujenzi wa shule mpya za awali na msingi katika maeneo ya kimkakati. Mwongozo wa ujenzi wa shule pia utahuishwa ili kuimarisha viwango vya ubora, usalama na manunuzi.

Mwaka 2-5: Ofisi ya Rais TAMISEMI itajenga angalau vyumba vya madarasa 12,000 (na kuweka vifaa vinavyohusika) kwa mujibu wa Mpango wa Uendelezaji wa Miundombinu ya Shule. Kwa kila vyumba vya madarasa viwili vinanavyojengwa, tundu moja la choo cha shimo litajengwa. Mamlaka za Serikali za Mitaa na shule zitatumia utaratibu wa Force Account na kushirikisha jamii kwa kuzingatia viwango na miongozo ya Serikali kuhusu ulinzi na viongozi. Kila mwaka Serikali inapaswa kupanga kujenga vyumba vya madarasa visivyopungua 3,000 pamoja na kuweka vifaa vinavyohusika

DLI 2: Utekelezaji wa Mpango wa Shule za Msingi salama

Mwaka 1: Wizaraya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI zitaidhinisha Mpango wa Shule ya Msingi salama (PSSP) na kuchagua shule 6,000 zitakazotekeleza mpango huo. Mpango huo utatekelezwa kwa kuzingatia mifumo iliyopo ya shule salama na inajumuisha yafuatayo:

Mwaka 2-5: Shule zitatekeleza PSSP kuhakikisha angalau asilimia 70 ya programu inatekelezwa kikamilifu. Serikali itafikia shule za msingi 1,000 katika Mwaka wa 2, shule 2,500 mwaka wa 3 (jumla), shule 4,500 mwaka wa 4 (jumla), na jumla ya 6,000 katika Mwaka wa 5.

DLI 3: Kuongezeka kwa asilimia ya Uwiano wa Uandikishaji wa Wanafunzi wa Elimu ya Awali

Mwaka 1-5: Malipo yataendana na ongezeko la asilimia ya uwiano ghafi wa kitaifa (GER) wa uandikishaji wa wanafunzi katika madarasa ya Elimu ya Awali. Mafanikio ya utekelezaji wa DLI 1 yatasaidia kufikia DI hii. Serikali pia inahimizwa kubuni mikakati ya kuongeza uandikishaji wa wanafunzi wa Elimu ya Awali bila kuathiri viwango vya Ubora.

DLI 4: Utekelezaji wa njia bora na matumizi ya vifaa Stahiki vya kufundishia na kujifunzia katika Madarasa ya Elimu ya Awali

Mwaka 1: Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI zitaidhinisha mpango stahiki kwa ajili ya ufundishaji na ujifunzaji wa Elimu ya Awali na programu ya mafunzo ya walimu wa Elimu ya Awali. Programu ya mafunzo ya walimu itaandaliwa naTaasisi ya Elimu Tanzania kwa kushauriana na wadau na kuendeleza program zilizopo za Elimu ya Awali zilizoonesha mafanikio.

Mwaka 2-5: Serikali itatekeleza mpango wa uboreshaji wa Elimu ya Awali na mafunzo ya walimu katika madarasa 12,000 ya Elimu ya Awali (katika shule mbalimbali) ili kuwezesha ufundishaji na ujifunzaji.

DLI 5. Halmashauri zinatekeleza Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA) katika ngazi za Shule na kupitia vituo vya Walimu

Mwaka 1-5: Serikali itatekeleza Mpango wa Taifa wa Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA). Utaratibu mpya wa MEWAKA utasimamiwa na Halmashauri ambapo ngazi kuu ya utekelezaji ni shule ikisaidiwa na Kituo cha Walimu ambavyo vimeboreshwa kwa kuwa na vifaa mbalimbali vikiwemo vifaa vya TEHAMA Utekelezaji wa MEWAKA utafanywa kwa awamu: Mwaka wa 1 utahusisha Halmashauri 26, Mwaka wa 2 Halmashauri 52, Mwaka wa 3 Halmashauri 92, Mwaka wa 4 Halmashauri 118, na mwaka wa S Halmashauri 184.

DLI 6: Idadi ya Shuleza Msingi na Vituo vya Walimu (TRC) Vinavyotekeleza mtaala wa TEHAMA katika kufundishia na kujifunzia vinavyowezeshwa kupitia mfumo wa Usimamizi wa Ujifunzaji

Mwaka 1: Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI zitaidhinisha kiunzi cha ujuzi wa kidijitali kwa Shule za Msingi na mpango wa Mafunzo ya TEHAMA kwa walimu na wanafunzi. Hii itaandaliwa kwa kuzingatia Sera na Mkakati wa TEHAMA katika Elimu. Serikali itachagua angalau Shule za Msingi 800 kunufaika na Mpango huu.

Mwaka 2-5: Serikali itatekeleza Mpango wa Mafunzo ya TEHAMA katika Shule za Msingi zisizopungua 800 kote nchini na kufuatilia utekelezaji wake. Lengo kuu ni kuwa na angalau Shule moja ya Msingi katika kila Kata nchini Tanzania inayotekeleza mpango wa mafunzo ya TEHAMA ili kusaidia utekelezaji wa MEWAKA na ufundishaji na ujifunzaji.

DLI 7: Utengaji wa bajeti kwa ajili ya Kuwezesha shughuli muhimu za Programu na kuhakikisha kuwa kiwango cha bajeti kinadumishwa au kuongezwa

Mwaka 1-5: Kila mwaka Serikali itatoa bajeti Stahiki kwa Elimu ya Awali na Msingi, ikijumuisha ruzuku ya Elimu bila Malipo kwa wanafunzi, MEWAKA, ukarabati wa shule na matengeo mengine muhimu ya bajeti, kwa kuzingatia kiunzi cha matumizi ya programu ya BOOST ili kuhakikisha mpango mzima wa programu unatekelezwa.

DLI 8: Idadi ya Halmashauri zinazokidhi vigezo vya Utawala bora katika Elimu

Mwaka 1: Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI zitaidhinisha Mwongozo wa Utawala Bora katika Elimu wa Halmashauri na Mwongozo wa Usimamizi wa Shule. Mwongozo wa Utawala Bora katika Elimu wa Halmashauri utajumuisha uwekaji wa mipango, usimamizi wa shule, ukaguzi wa ndani, usimamizi wa ujenzi, ushirikishwaji wa jamii na ushughulikiaji wa malalamiko. Mwongozo wa Usimamizi wa Shule utaandaliwa kutokana na miongozo iliyopo lakini utaboreshwa ili kujumuisha usimamizi wa MEWAKA, Programu ya Shule Salama, na jitihada mpya.

Mwaka 2-5: Serikali itaendelea kutoa mafunzo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na shule na kufuatilia uzingatiaji wa Mwongozo wa Utawala Bora katika Elimu wa Halmashauri na Mwongozo wa Usimamizi wa Shule.

USIMAMIZI WA PROGRAMU NA MSAADA WAKITAALAMU

  • BOOST inatenga dola za Marekani Milioni 20 kugharamia usimamizi wa Programu, ushauri wa kitaalamu, na kujenga uwezo wa Taasisi za Serikali zinazotekeleza mradi, ikiwa ni pamoja na Halmashauri ili kufikia vigezo vilivyowekwa (DLIs).
  • Usaidizi wa kipekee wa kitaalamu utatolewa kwa TIE, NECTA, na TSC ili kuendeleza uwezo wao wa kimsingi katika ukuzaji wa mtaala, upimaji wa ujifunzaji, na katika uundaji na utekelezaji wa sera za walimu.
  • Uongozi na usimamizi wa shule katika ngazi za Mikoa na Serikali za Mitaa utaimarishwa kupitia programu za mafunzo zinazoratibiwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI

MPANGO WA UTEKELEZAJI

Timu ya Kitaifa ya Utekelezajiwa Mradi (NPIT) imeanzishwa ikiwa na waratibu kutoka WYEST na OR-TAMISEMI, inajumuisha wataalam wa usimamizi wa fedha, ununuzi, ulinzi na usalama, na ufuatiliaji na tathmini. NPIT inawajibika kusimamia na kuratibu utekelezaji wa BOOST katika ngazi ya kitaifa na itaitisha mara kwa mara Vikundi Kazi vya Maudhui ya DLI ili kuhakikisha upangaji na utekelezaji wa programu. NPIT pia itawezesha mikutano ya Kamati ya Uongozi wa Mradi na Kamati ya Kitaalamu na kufanya kazi kwa karibu na Benki ya Dunia Washirika wengine wa Maendeleo.

Timu ya Utekelezaji wa Mradi katika ngazi ya Halmashauri (LPIT) imeanzishwa katika kila Halmashauri. LPIT itaongozwa na Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri (DEO) wa na kusaidiwa na timu inayojumuisha Mthibiti Ubora wa Shule, wawakilishi kutoka Maafisa Elimu Kata, walimu wakuu, Idara za fedha, manunuzi, ustawi wa jamii, na maofisa maendeleo ya jamii katika Halmashauri, LPIT itakuwa na jukumu la kuandaa mipango kazi ya kila mwaka na bajeti, usimamizi wa ujenzi unaoshirikisha jamii, kuratibu utekelezaji wa MEWAKA na programu ya Shule ya Msingi salama na kufuatilia utekelezaji wa programu katika shule zilizopo ndani ya Halmashauri.

Ratiba ya Mradi

Ili kufikia vigezo vilivyowekwa (DLIs) kila mwaka, taasisi zote zinazotekeleza zitahitajika kupanga bajeti ya kutosha kwa ajili ya shughuli zilizopangwa na kusimamia utekelezaji wake. DLIs zitathibitishwa na Wakala Huru wa Uthibitishaji (IVA). Baada ya kuthibiti shwa kwa matokeo hayo, kiasi cha fedha kinacholingana na kiwango cha matokeo yaliyothibitishwa kitatolewa kutoka Benki ya Dunia kwenda kwa Serikali ya Tanzania. Mzunguko wa upangaji bajeti, utekelezaji, uthibitishaji wa matokeo, na ulipaji utaendelea katika muda wote wa Mradi.