Majukumu ya Kitengo cha Huduma za Sheria

Kwa kuzingatia Muundo wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (Function and Organizational Structure for the Ministry of Education, Science and Technology), Kitengo cha Huduma za Sheria kina majukumu mahsusi yafuatayo:

a) Kutoa huduma na msaada wa kisheria kwa Idara na vitengo vya Wizara kuhusiana na tafsiri ya sheria, masharti ya mikataba, masharti ya makubaliano, mikataba ya ununuzi, n.k;

b) Kutoa ushauri wa kiufundi katika uandaaji wa nyaraka mbalimbali za sheria na kuziwasilisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali; 

c) Kutoa huduma za kisheria kwa Wizara na Taasisi zake;

d) Kushiriki katika majadiliano na mikutano mbalimbali ambayo inahitaji ushauri au utalaam wa kisheria katika masuala yanayohusu sekta ya elimu;

e) Kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kuendesha mashauri ya madai na mashauri mengine yanayohusu Wizara; na

f) Kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kupitia nyaraka mbalimbali za kisheria zikiwemo Amri, Matangazo ya Serikali, Mikataba, Makubaliano n.k.

 

SHERIA YA ELIMU, SURA YA 353

SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023 (SWA&ENG)