Wizara, imeanza kutumia mfumo wa kielektroniki wa kukusanya mapato ya Serikali kwenye makusanyo yake yote ya mapato kwa Vyuo vya Ualimu vya Serikali, Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi na Kanda za Uthibiti Ubora wa Shule. Hivyo mteja atapaswa kufika au kuwasiliana na kituo husika anachotaka kufanya malipo ili kupata namba ya utambulisho wa malipo husika (Payment Control Number) kabla ya kufanya malipo
1. Malipo yanaweza kufanywa kwa njia ya kibenki kwa kufuata hatua zifuatazo;
- Unapopata kumbukumbu ya malipo (Control Number);
- Tembelea Tawi lolote la Benki ya CRDB, NMB na NBC;
- Baada ya kuwasili kwenye benki, mpe mtoa huduma wa dirishani namba kumbukumbu ili kukamilisha mchakato wa malipo yako.
2. Malipo yanaweza pia kufanywa kwa njia ya mtandao wa simu za mikononi (M-pesa, Tigo Pesa na Airtel Money) kwa kufuata hatua zifuatazo;
- Kupitia simu yako, piga *150*00#, au *150*01# au *150*60#;
(Kupitia M- pesa, Tigo Pesa na Airtel Money);
- Chagua ‘Lipia malipo (Pay-Bills)’;
- Chagua ‘Malipo ya Serikali’;
- Chagua ‘Ingiza namba ya malipo’ na uingize namba ya kumbukumbu ya malipo (Control Number);
- Weka kiasi cha fedha unachotaka kulipa;
- Thibitisha muamala wako kwa kuingiza neno au namba yako ya siri; na
- Hifadhi ujumbe wa simu uliopokea kama ushahidi wa malipo endapo utahitajika kuonyesha kwa kituo husika.