TARATIBU ZA KUANZISHA NA KUSAJILI SHULE

Ili kuanzisha na kusajili Shule yenye ubora unaostahili wadau hawana budi kufuata hatua mbalimbali kama zilivyoainishwa kwa kina katika “Mwongozo wa Usajili wa Shule wa mwaka 1982”.  Kwa kifupi hatua hizo ni kama.

[accordion] [acc_item title="Hatua ya kwanza:  Kibali cha  Kujenga Shule"]

Mwenye nia na uwezo wa kuanzisha Shule atume maombi ya kutaka kujenga shule kwa maandishi kwa Afisa Elimu

Kiongozi.  Maombi haya yapitishwe kwa Afisa Elimu  wa Wilaya Shule itakapojengwa na Afisa Elimu  Mkoa yakiwa na viambatisho vifuatavyo: 

  • Rejea mwongozo wa andiko la mradi la Wizara, Bank Statement yenye zaidi y ash. Milioni 62,000,000/=  Nakala ya hati/offer/uthibitisho wa kumiliki ardhi iliyotolewa kwa matumizi ya shule inayotambu8lika kisheria na serikali kuu ya mtaa au kijiji ( eneo lisipungue ekari 71/2  kijijini na 31/2 mjini) Michoro ya majengo ya shule inayoonyesha vipimo kwa kuzingatia viwango vya Wizara na Elimu ya mafunzo ya ufundi, Ramani ya shule inayoonyesha mpangilio wa majengo na viwanja vya michezo, Cheti cha usajili wa kampuni, shirika , umoja , NGO iwapo shule ni ya jumuia na katiba yake au mkataba wa maridhiano. Endapo mdau anataka ikutumia jina la Mtakatifu ( Saint ) awasilishe kibali toka kwa askofu wa dini inayotambulika kinachoidhinisha matumizi ya jina hilo.
  • Kamishina wa Elimu akiridhika na maombi hayo atatoa kibali cha kujenga Shule kimaandishi, ndipo ujenzi utaanza.

[/acc_item] [acc_item title="Hatua ya pili: Kuthibitishwa kuwa Mwenye Shule na Meneja wa Shule"]

Hatua hii ni kwa wale tu waliokamilisha hatua ya kwanza na inahusisha yafuatayo:

  • Mwombaji ajaze fomu Na. RS. 6 ya kuomba kuthibitishwa kuwa Mwenye Shule na RS. 7 ya kuomba kuthibitishwa kuwa Meneja wa Shule.  Hatua hii itafanywa baada ya mwombaji kuwa amekamilisha ujenzi wa majengo yote  muhimu kwa asilimia 75% Majengo hayo ni vyumba vya madarasa, Jengo la utawala/Ofisi za walimu, Maktaba, vyoo vya wasichana, wavulana na wafanyakazi bwalo/ukumbi,  maabara. Majengo hayo lazima yawe yamekaguliwa na mamlaka za Wilaya, ambazo ni ; Mhandisi wa Majengo , Afisa Afya na Mthibiti Mkuu wa Ubora wa Shule wa Wilaya na kwamba fomu hizo ziwe zimepitishwa na  Afisa  Elimu wa Wilaya, Afisa Elimu wa Mkoa na  Katibu Tawala wa Mkoa.
  • Wizara ikiridhika itatoa kibali cha maandishi cha kumthibitisha Mwenye Shule na Meneja wa Shule.

Hatua hii ni kwa wale tu waliokamilisha hatua ya kwanza na ya pili na inahusisha yafuatayo:

  •  Mwenye Shule hujaza fomu Na. RS 8 ya maombi ya kusajili shule baada ya kuwa amekamilisha mahitaji yote yanayotakiwa kwa Shule ya aina anayoiomba: ambayo ni  Majengo na Samani, Vitabu, Mihutasari ya masomo, Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia na Kuajiri walimu na wafanyakazi wengine wenye sifa na uzoefu.
  • Mwenye Shule ambaye Shule yake imetimiza vigezo vyote na shule kukaguliwa na Mkaguzi Mkuu wa Shule wa Kanda hupewa taarifa ya kusajiliwa kwa Shule yake kimaandishi.  Aidha, atapatiwa cheti cha usajili chenye namba ya usajili .

Usajili wa Shule za Kimataifa

Wizara husajili shule zenye hadhi ya kimataifa, usajili huo unafanywa na Taasisi za kimataifa zinazosajili Shule za aina hiyo.  Wizara huthibitisha na kutambua shule zinazosajiliwa na taasisi hizo kama za kimataifa.  Taasisi hizo ni “European Council for International Schools” (E.C.I.S) na “Association of International Schools in Africa (AISA).  Taasisi hizo zimeweka vigezo vya

kusajili Shule za kimataifa.  Shule itapewa usajili pale tu itakapotimiza vigezo vyote vilivyowekwa.

Hatua za kufuata ili Shule iwe ya Kimataifa

Mwenye Shule yeyote anayetaka Shule yake iwe na hadhi ya kimataifa anapaswa kufuata hatua zifuatazo:

  • Shule isajiliwe na Wizara kama shule ya kawaida.
  • Mwenye Shule aiombe Wizara kimaandishi kutaka Shule yake iwe ya kimataifa.
  • Endapo Wizara itaridhika na ombi hilo itatoa kibali cha maandishi na Mwenye Shule ataendelea na hatua za kutuma maombi kwenye taasisi zinazosajili shule hizo.
  • Shule itakaposajiliwa kama ya kimataifa, Mwenye Shule aijulishe Wizara kimaandishi na kuambatisha nakala ya usajili huo.

Usajili wa shule/Taasisi za kidini

Taasisi za kidini zinazotaka kuanzisha na kuendesha Shule/Taasisi za kidini zinapaswa kufuata hatua zote tatu kama zilivyoelezwa isipokuwa wanapaswa kujaza fomu Na. RS.9 katika hatua ya usajili.

Tanbihi

Uvunjaji wa Sheria kwa namna yoyote ile ni kosa la jinai na adhabu yake ni kama ilivyofafanuliwa katika Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 kifungu cha 59.

Ni nani anayehusika katika mchakato wa usajili wa shule?

  • Katika ngazi ya Wilaya:

Wakaguzi wa Shule; Maafisa Elimu; Wahandisi wa Majengo na Maafisa Afya wana wajibu mkubwa wa kuthibitisha kuwa maandalizi ya kutosha kuhusu majengo na mazingira ya Shule kiafya yanafaa kwa matumizi ya shule.  Taarifa zinazoandaliwa na watendaji hao husaidia kutoa picha halisi ya matayarisho na kutoa mapendekezo sahihi pale wanapopitisha fomu za maombi ya kumiliki na kuendesha shule.  Maombi haya huisaidia Wizara kupata picha halisi kuhusu matayarisho ya mwombaji na kufanya uamuzi sahihi.

  • Watendaji wa Serikali ya Kijiji/Mtaa na Kata

Hutoa taarifa mahsusi zinazosaidia kutoa picha ya mahitaji ya Elimu katika eneo lao na kumthibitisha anayetaka kuanzisha Shule kama ndiye mmiliki halali wa eneo la Shule itakapojengwa.

  • Mkaguzi Mkuu wa Shule wa Kanda

Hufanya ukaguzi maalumu kwa lengo la kusajili shule na hukamilisha fomu Na RS. 8 kisha kutuma fomu hizo kwa Kamishina wa Elimu pamoja na taarifa ya Ukaguzi wa Shule husika.  Mkaguzi Mkuu wa Shule husimamia na kutathimini utekelezaji wa mitaala pamoja na uendeshaji wa shule kwa ujumla.

  • Katibu Tawala wa Mkoa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya

Husimamia masuala yote ya maendeleo ya Elimu katika maeneo yao.  Wanajukumu la kutoa maamuzi juu ya aina ya mipango inayotakiwa kufanywa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule za serikali za msingi na za sekondari.  Wanasimamia uhamasishaji wa maendeleo ya sekta ya elimu ya jamii inayowazunguka pia wanapokea na kupendekeza maombi ya kutaka kumiliki, kuendesha na kusajili Shule.

  • Waziri wa Elimu,

Waziri wa Elimu humthibitisha Mwenye Shule na huidhinisha usajili wa Shule za dini.

Usajili wa walimu unafanywa kwa mujibu wa Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 sehemu ya VI na rekebisho lake Na. 10 la mwaka 1995 pamoja na Kanuni ya Elimu ya mwaka 2002.

Makundi matatu ya walimu yanayoweza kusajiliwa

  • Mwalimu aliyefuzu na kufaulu mitihani kutoka katika chuo kinachotambulika na Serikali.
  • Mtu asiye na taaluma ya Ualimu atakayeomba na kupatiwa leseni ya kufundisha.
  • Walimu wasio raia wa Tanzania waliofuzu taaluma ya Ualimu wanaoomba na kupatiwa leseni ya kufundisha.

Walimu wenye sifa

  • Mwalimu mwenye sifa husaini mkataba na mwajiri wake kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi za Walimu za mwaka 2003
  • Mwalimu huyu husajiliwa kutoka rejesta Na. II kama mwalimu anayesubiri kuthibitishwa.
  • Baada ya kumaliza muda wa kusuburi kuthibitishwa kwa mwaka mmoja,  mwalimu huthibitishwa kwenye rejesta Na. I ya walimu waliothibitishwa kazini.

Walimu walio na taaluma ya ualimu ambao sio watanzania wanaotaka kufundisha nchini

  • Mwombaji ataomba kupatiwa leseni ya kufundisha kupitia kwa uongozi wa shule anayotaka kufundisha na kuyapitisha maombi hayo kwa Mthibiti Mkuu wa Ubora wa Shule wa Kanda.  Mwombaji anaambatisha vyeti vya taaluma na umri wake.
  • Mthibiti Mkuu wa Ubora wa Shule wa Kanda. hupitia na kutoa mapendekezo ya maombi hayo kwa Kamishina wa Elimu
  • Maombi ya ajira ya Walimu huchambuliwa na kamati maalum ambayo mwenyekiti wake ni Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala kisha humshauri Waziri kupitisha maombi haya.
  • Waziri akiridhika hutoa kibali cha kufundisha nchini.
  • Kamishina wa Elimu  hutoa idhini ya mwombaji kupatiwa leseni.
  • Walimu wenye leseni wanasajiliwa kwenye rejesta Na. III

Mwongozo wa Usajili wa Shule wa mwaka 1982 unapatikana katika Ofisi za Elimu za Wilaya, Mkoa na Makao Makuu ya Wizara.  Mwongozo huu unatoa tafsiri ya Sheria ya Elimu na Kanuni za Elimu kuhusu usajili wa shule na walimu.

Mambo muhimu yaliyopo katika mwongozo ni pamoja na fomu za usajili wa shule na walimu.  Aina ya fomu (majina mapya katika mabano) hizo ni:

  • Fomu Na.6 (RS 6) kuhusu maombi ya kutaka kuwa Mwenye Shule na fomu Na. 7 (RS 7) kuhusu maombi ya kutaka kuwa Meneja wa Shule.
  • Fomu Na. 8 (RS 8) kuhusu maombi ya usajili wa shule zisizo za Serikali na Fomu Na. 9 (RS 9) kuhusu maombi ya leseni na usajili wa Shule/Taasisi za Dini.
  • Fomu Na. 4 (RT 4) kuhusu maombi ya kutaka kupatiwa leseni za kufundisha.
  • Fomu Na, 3 (RS 3) kuhusu taarifa ya kusajiliwa walimu wenye leseni katika rejesta Na. 3
  • Fomu Na. 1 (RT 1) kuhusu cheti na taarifa ya kusajiliwa walimu ambao wamemaliza muda wa mwaka mmoja na kusubiri kuthibitishwa kazini. 

BONYEZA HAPA KUPATA MFUMO WA USAJILI WA SHULE