-->

Mpango wa Mafunzo ya INSET

18 Julai 2016

Ufundishsaji wa Hisabati na masomo ya Sayansi (Biology, Chemistry na fizikia) umekuwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na uhaba wa walimu, walimu wenye uwezo mdogo, uhaba wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia, ukosafu wa vifaa, madawa, maabara

kutokamilika.  Hali hii imesababisha masomo kwa vitendo kukosa ufanisi stahiki na kusababisha Waalimu kutofundisha ipasavyo masomo ya vitendo kuwa nadharia jambo lililoshusha ufaulu katika mitihani, na kupunguza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na michepuo ya Sayansi.

Hali hii imeonyesha umuhimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati kwa walimu wa Sekondari, Wizara ya Elimu (WESTU) kwa ushirikiano na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) wanaendesha mafunzo kazini kwa walimu wa Sayansi, Hisabati na Lugha ya Kiingereza kwa madhumuni ya kuongeza ufanisi wa walimu ili kiwango cha ufundishaji na ujifunzaji vipande.

Lengo Kuu

Lengo la mafunzo ni kupandisha ubora wa ufundishaji Sayansi, Hisabati pamoja na Lugha ya Kiingereza kwa ngazi zote za elimu ya Sekondari hpa nchini.

Dhumuni

Kuimarisha mpango wa mafunzo kazini (INSET) kwenye mfumo wa Elimu ya Sekondari kwenye mafunzo ya Sayansi, Hisabati na Walimu wa Lugha ya Kiingereza.

Matokeo

Mafunzo kazini yameanzishwa kwa kufuata moduli zilizoandaliwa kama iifuatavyo:-

AINA ZA UTARATIBU WA KUENDESHA MAFUNZO (A cascade)

Utaratibu wa mpangilio wa mafunzo ni kama ufuatavyo:-

Wakufunzi wa ngazi ya Taifa huchaguliwa toka Walimu Wakuu wa Mikoa, hupatiwa mafunzo, wakishamaliza nao hutoa mafunzo ya walimu waliochaguliwa wakihitimu masomo yao huitwa Wakufunzi wa ngazi ya Mkoa (RT), nao hutoa mafunzo kwa kundi jingine ambao wataitwa Wakufunzi wa Wilaya (DR), ambao wao watafundisha Walimu wa Sayansi, Hisabati na Kiingereza waliopo katika Wilaya yao.  Kimpangilio mafunzo ya INSET huanzia juu na kushuka chini.

Jukumu la Ngazi mbalimbali za Mpango wa Mafunzo ya INSET kwa Walimu wa Masomo ya Sayansi, Hisabati na Kiingereza

i. Kamati (hukutana mara moja kwa Mwaka wa Fedha) Shughuli za Kamati Shirikishi

 • Kuhakiki na kupitisha shughuli(plan) za mpango
 • Kufanya mapitio ya maendeleo ya shughuli za mpango
 • Kuandaa maamuzi ya sera kwa kurejea uimarisho wa mipango ya shughuli za inset kwa shule za Sekondari kwa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati.

Muhtasari wa Kamati Shirikishi

 Committee

ii. Kitengo cha Uratibu Kitaifa

Majukumu

 • Kuandaa mwongozo wa utekelezaji wa shughuli za INSET kama inavyotakiwa
 • Kufanya ufuatiliaji na upimaji wa mpango wa mradi
 • Kuandaa taarifa ya utekelezaji na kukabidhi Kamati Shirikishi
 • Kuendesha shughuli za mradi kwenye ngazi ya Mkoa kwa mashirikiano na jopo la Mkoa kiutawala
 • Kuhamasisha wadau ili wauwezeshe mradi kufanya kazi
 • Ufuatiliaji upatikanaji wa fedha za utekelezaji shughuli za mradi
 • Kuandaa mpango kazi wa mradi
 • Kuratibu shughuli za mradi

iii. Kamati ya Kitaalamu Kitaifa (hukutana mara mbili kwa mwaka)

Majukumu

 • Kuweka viwango vya mpango wa mafunzo
 • Kuandaa miongozo vitini na vijarida vya kufundishia na kujifunzia

iv. Kamati ya Kitaalam ya Mkoa (hukutana mara mbili kwa mwaka)

Majukumu

 • Inawajibika katika utekelezaji wa shughuli za mradi ngazi ya Mkoa
 • Kupitisha mpango kazi ulioandaliwa na Kamati ya Kitaalamu ya Mkoa
 • Kutafuta fedha, kuzigawa na kuzisambaza kama ilivyokusudiwa
 • Kuhakikisha mafunzo kazini ya Walimu ngazi ya Mkoa yanaendeshwa vizuri kwa kufuata mihula (Schedule) ilivyopangwa
 • Kukabidhi taarifa ya utekjelezaji kwa mratibu wa mafunzo Kitaifa katika kitengo husika (WESTU& RALG)

Wahusika kwa Wadhifa:

 • Mwakilishi toka (CWT) Chama cha Walimu.
 • Mwakilishi wa TAMONGOSCO
 • Mthibiti ubora wa Elimu wa Kanda
 • Wawakilishi watatu ambao ni Wakuu wa shule
 • Afisa Elimu wa Wilaya (Sekondari) toka Halmashauri zote
 • Afisa Elimu wa Mkoa  – Mwenyekiti

v. Kamati ya Mkoa ya Kitaalam (hukutana mara mbili kwa mwaka)

Majukumu

 • Kuandaa mpango kazi wa mwaka na kuukabidhi kwa Kamati ya Mkoa.
 • Kuandaa na kukabidhi Taarifa kwa Kamati ya Mkoa

Wahusika kwa Wadhifa

 • Afisa Taaluma wa Elimu (Mkoa) (Sekondari Education) Mwenyekiti
 • Afisa Elimu Wilaya SEKONDARI WOTE
 • Wakuu wa Shule – wenye vituo vya Mafunzo
 • Uwakilishi wa wakufunzi wa Mkoa (RF) kwa kila somo
 • Wathibiti ubora wa Elimu waliotoka kanda mbili tofauti (Science & math).

Video News

Contact

 • Name:    Permanent Secretary
 • Address: 
 •               Mtaa wa Afya - Mtumba
 •               P.O.Box 10
 •               Dodoma
 • Tel:        +255 26 296 3533
 • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
 • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…